Thursday, July 12, 2012

WALIMU WAMSHUSHUA WAZIRI KASSIM MAJALIWA

Rais wa CWT, Gratian Mukoba

RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, ameibuka leo na kupinga taarifa iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa, aliyesema kwamba walimu hawana mgogoro wowote na serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mukoba amesema kwamba kauli hiyo ya serikali bungeni si ya kweli kwani hivi sasa wana mgogoro na serikali kuhusiana na madai yao mbalimbali.

Amefafanua kuwa mgogoro wao na serikali ulisainiwa tangu Juni 8 mwaka huu na kwamba, majadiliano yao na serikali hayajafikia muafaka baada ya wenzao (serikali) kuomba kuahirisha hadi Julai 20.

Akaongeza kuwa, kama wakishindwa kuafikiana katika kikao chao kinachofuata, watasaka idhini ya kuchukua hatua zaidi.

Mukoba aliita taarifa hiyo ya serikali kuwa ni ghilba na kwamba kamwe haiwezi kuwasaidia walimu waliokosa mshahara na pia  hazitasaizidi kuinua morari ya walimu waliokata tamaa. Akasisitiza kwamba cha muhimu ni kutanguliza ukweli na sio ghilba.

Hata hivyo, aliwataka walimu kuendelea na kazi katika kipindi hiki wanachoendelea kuzungumza na serikali.
.

No comments:

Post a Comment