Simba na Yanga mpo? Tazama liuwanja la Santiago Bernabeu linavyoonekana kwa nje. |
Hivi ndivyo 'liuwanja' la Santiago Bernabeu linavyoonekana sasa kwa juu. |
'Liuwanja' la uwekli la Santiago Bernabeu linavyoonekana kwa ndani. |
Hapa 'liuwanja' la Santiago Bernabeu linavyoonekana kwa ndani katika engo tofauti. |
Liuwanja la Santiago Bernabeu linavyoonekana kwa ndani baada ya kujaa mashabiki. |
MADRID, Hispania
Real Madrid imeripotiwa kuwa inafikiria kuupa jina jingine uwanja
wake wa Santiago Bernabeu ikiwa ni sehemu ya makubaliano waliyofikia na
mdhamini Emirates.
Kwa mujibu wa ABC, Real hawako tayari kutekeleza wazo la
kuondosha kabisa jina la awali la uwanja ambalo ni la rais gwiji wa klabu hiyo.
Hata hivyo, hawapingi jina hilo kutanguliwa na la kampuni inayowadhamini.
Kwa sababu hiyo, Emirates, ambayo hivi karibuni imeingia
mkataba wa miaka mitano wa kudhamini jezi za Real, sasa inatoa ofa ya kuongeza
euro milioni 53 katika kila msimu ili kubadili jina la kiwanja kimojawapo
maarufu cha soka duniani na kuitwa 'Fly-Emirates-Bernabeu'.
Kadri ya hali ilivyo sasa, shirika hilo la ndege lenye
maskani yake mjini Dubai, na ambalo hivi sasa lina haki za jina la uwanja wa Arsenal,
litakuwa na haki ya kuona kuwa logo ya kampuni yake ikitumika katika jezi za
Real Madrid kuanzia mwaka 2013 na kuendelea.
Uwanja wa Santiago Bernabeu ulizinduliwa mwaka 1947 na, kufuatia
upanuzi wake mwaka 2011, sasa una uwezo wa kuchukua watazamaji 85,454.
No comments:
Post a Comment