Monday, July 30, 2012

TUNDU LISSU ASIKITIKIA KUFUNGIWA GAZETI LA MWANAHALISI


*AWATETEA PIA MADAKTARI WALIOFUTIWA USAJILI

Ukurasa wa mbele wa moja ya nakala za gazeti la Mwanahalisi.

Mbunge wa Iramba Mashariki, Mhe. Tundu Lissu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu, ameonyesha kusikitishwa na uamuzi uliotolewa leo na serikali wa kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la kila wiki la Mwanahalisi.



Mheshimiwa Lissu amezungumzia masikitiko yake hayo jioni hii kabla hajaanza kuchangia mjadala kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka ujao wa fedha.



Lissu alisema kwamba kwa watu wote wanaojua maana ya uandishi wa habari za kiuchunguzi, taarifa za kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ni sawa na giza nene.

“Kwa wanaofahamu 'Investigative Journalism (uandishi wa habari za uchunguzi), kufungiwa kwa Mwanahalisi kwao ni giza...,” alisema Mhe. Lissu.



Hata hivyo, kabla Mhe. Lissu hajaeleza zaidi juu ya namna alivyoguswa na uamuzi huo wa serikali, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, alimkatisha na kumtaka ajielekeze katika kuchangia hoja iliyoko mbele yao kwa wakati huo; raia ambayo Mhe. Lissu aliifuata na kuanza kujadili juu ya suala la kutimuliwa kwa madaktari hali ya huduma za afya nchini.



Leo, serikali imetangaza kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kitendo cha gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari na makala za uchochezi.


KUTIMULIWA KWA MADAKTARI


Katika kuchangia kwake, Lissu alisema kwamba inasikitosha kuona kuwa hivi karibuni serikali imewafutia usajili madaktari zaidi ya 300 huku ikijua wazi kwamba taifa lina upungufu mkubwa wa watu hao.



Akasema kuwa ni vyema serikali ikaangalia uwezekano wa kuboresha maslahi ya kada hiyo na si kuwafukuza pale wanapodai haki zao na kuwafanya wengine waende kutumika katika maeneo mengine wanakothaminiwa zaidi na kulipwa vizuri kama Botswana.



“Inakuwaje tunatumia fedha nyingi kusomesha madaktari, halafu tunawaachia wakatumikie nchi nyingine kama Botswana?” alihoji Mhe. Lissu.



Akieleza zaidi, Mhe. Lissu akasema kuwa madaktari waliofukuzwa (baada ya kugoma) hawakutendewa haki kwa vile hawakupewa nafasi ya kujitetea, na kwamba uamuzi huo pia ni kosa kwa mujibu wa sheria.




“Huwezi kushughulikia tatizo la uvunjifu wa sheria, kwa kuvunja sheria... uongo mara mbili hautengenezi ukweli mmoja,” alisema.


No comments:

Post a Comment