Monday, July 30, 2012

TAZAMA KITIMTIM CHA MPIRA WA WAVU WA UFUKWENI KWENYE MICHEZO YA OLIMPIKI JIJINI LONDON LEO

Hana Klapalova (kulia) na Lenka Hajeckova (kushoto) wa Jamhuri ya Czech wakishangilia huku Natacha Rigobert wa Mauritius  akipiga goti mchangani baada ya mechi yao ya leo ya hatua za awali za mpira wa wavu wa ufukweni katika michezo ya Olimpiki ya London 2012 kwenye viwanja vya Horse Guards Parade.

Hana Klapalova (kulia) na Lenka Hajeckova (kushoto) wa Jamhuri ya Czech wakiuwahi mpira mbele ya Nioun Chin Elodie Li Yuk Lo wa Mauritius wakati wa mechi yao ya leo ya hatua za awali za michuano ya mpira wa wavu wa ufukweni katika michezo ya Olimpiki ya London 2012 kwenye viwanja vya Horse Guards Parade.
Mchanga ukirushwa wakati Hana Klapalova Jamahuri ya Czech akijaribu kurudisha mpira dhidi ya Mauritius.


Lenka Hajeckova wa Jamhuri ya Czech akipiga mpira katika mechi yao dhidi ya Mauritius kwenye viwanja vya Horse Guards Parade leo.
Hana Klapalova wa Jamhuri ya Czech akipiga mpira huku mwenzake Lenka Hajeckova (kushoto) akimtazama wakati wa mechi yao ya mpira wa wavu wa ufukweni dhidi ya Mauritius katika michezo ya Olimpiki London 2012 kwenye viwanja vya Horse Guards leo.  

Hana Klapalova wa Jamhuri ya Czech akiokoa mpira katika mechi yao dhidi ya Mauritius.Nioun Chin Elodie Li Yuk Lo wa Mauritius (kushoto) akirudisha mpira wakati mchezaji mwenzake Natacha Rigobert akimtazama wakati wa mechi yao dhidi ya Jamhuri ya Czech kwenye viwanja vya Horse Guards Parade leo.
Nioun Chin Elodie Li Yuk Lo wa Mauritius akishindwa kuanzisha vyema mpira katika mechi yao ya mpira wa wavu dhidi ya Jamhuri ya Czech leo.

No comments:

Post a Comment