Thursday, July 19, 2012

TOBAAA…! BIKINI ZA KIBRAZILI RUKSA MICHUANO YA MPIRA WA WAVU UFUKWENI MICHEZO YA OLIMPIKI LONDON


Lahaulaa...! Eti hapa madada walioshinda wanapongezana.

Jennifer Kessy (kushoto) akijaribu kuzuia mpira unaopigwa na Kerri Walsh. Timu ya Kessy ilishinda 2-0.

Holly McPeak na mwenzake Jennifer Kessy wakirudisha mpira uliopigwa na  Kerri Walsh na mwenzake Misty May-Treanor wakati wa kuwania taji la AVP Hermosa Beach Open kwenye fukwe za  Hermosa.

Nyota wa Marekani, Kerri Walsh na Misty May-Treanor wakipongezana.

Misty May-Treanor na Kerri Walsh (kushoto) wakikumbatiana kupeana moyo kabla ya kuwavaa Larissa Franca na Ana Paula Conelly wa Brazil

Hee... kumbe hata Rihanna yumo. Hapa anajiachia na mpira wa wavu kwenye fukwe za Ugiriki.

Tobaaa...! Sasa mchezo gani huu? Mcheki  Rihanna alivyojibinua kiuchokozi baada ya kunogewa na mpira wa wavu wa ufukweni wakati akiwa mapumzikoni Ugiriki.
LONDON, England
BIKINI za Kibrazili ni ruksa kutumika katika michuano ya mpira wa wavu ya ufukweni wakati wa michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini London kuanzia wiki ijayo.

Imeelezwa na waandaaji jijini London leo kuwa vivazi hivyo vya wachezaji vimeruhusiwa kwa vile ni miongoni mwa vivutio vikubwa kwa watazamaji.

Mchezo huo ulianza kujumuishwa rasmi kwa mara ya kwanza katika michezo ya Olimpiki kwenye fukwe za California mwaka 1996, lakini tangu wakati huo umekuwa ukipingwa na baadhi ya wahafidhina wanaohoji kitendo cha kuruhusu mchezo unaowaacha wanawake wakiwa na viguo vya kuogelea kuwemo katika ratiba ya Olimpiki.

Nchi za Marekani, Brazil na Australia ndizo hutawala zaidi katika mchezo wa mpira wa wavu wa ufukweni na ndio pekee hadi sasa zilizowahi kutwaa medali za dhahabu katika michuano ya Olimpiki huku wakali waliowahi kutwaa dhahabu mara mbili wakiwa ni pamoja na Wamarekani Misty May-Treanor, 34 na Kerri Walsh, 33.

No comments:

Post a Comment