Thursday, July 19, 2012

RAIS KIKWETE ATUA ZANZIBAR KUWAFARIJI WAHANGA WA BOTI ILIYOZAMA YA SKAGIT

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya boti ya Skagit iliyozama jana katika eneo la Chumbe, Zanzibar  wakati alipoongozana na mkewe Mama Salma Kikwete walipowatembelea manusura kwenye Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja leo.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea viwanja vya Maisara, Zanzibar leo ambako ndiko miili ya marehemu wa ajali ya boti ya Skagit hufikishwa kwa ajili ya utambuzi baada ya kupatikana baharini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakay Kikwete ameongozana na mkewe na kutua Zanzibar leo ili kuwafariji majeruhi na kuwapa pole watu waliofiwa na ndugu zao kufuatia msiba uliotokana na kuzama kwa boti ya Skagit kwenye eneo la Chumbe, Zanzibar.

Rais Kikwete aliwatembelea majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kabla ya kwenda kwenye viwanja vya Maisara ambako miili ya marehemu hufikishwa hapo na kutambuliwa na ndugu na jamaa

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Emmanuel Nchimbi, alifika pia visiwani Zanzibar leo na kuwataka wananchi wawe na subira na kuendeleza ushirikiano katika kipindi hiki cha kusaka zaidi miili ya watu waliozama na boti hiyo badala ya kuanza kunyoosheana vidole.

  

Waziri

No comments:

Post a Comment