Saturday, July 21, 2012

THIAGO SILVA: TUHUMA ZA KUJIANGUSHA HOVYO ZIMEMPONZA NEYMAR TUKIIFUNGA ENGLAND 2-0


Neymar of Brazil akishangilia penati aliyofunga wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na michezo ya Olimpiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England jana.
Neymar wa Brazil (kushoto) akichuana na Joe Allen wa timu ya Himaya ya Uingereza (GB) wakati wa mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na michezo ya Olimpiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England jana.
Ni mbwembwe tu, ubishoo au? Kama kawaida yake, yosso Neymar wa Brazil hakuacha staili ya kujibandika plasta juu ya pua wakati wakicheza dhidi ya Himaya ya Uingereza jana. 
LONDON, England
THIAGO Silva amefurahishwa na namna Neymar alivyoimarika na kuonyesha kiwango cha juu licha ya kupaniwa sana na mabeki na kuchapwa viatu vya hatari huku refa akiachia wakati timu yao ya taifa ya Brazil ikishinda 2-0 dhidi ya Himaya ya England katika mechi yao ya kirafiki kujiandaa na michezo ya Olimpiki kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough jana.

Silva alisema kuwa Neymar alichezewa faulo kadhaa za wazi walizopaswa kupewa ‘fri-kiki’ na penati, lakini refa ‘alizichuniwa’ kutokana na kile anachoamini kuwa ni ‘dogo’ huyo mwenye kipaji kuponzwa na uvumi kwamba huwa anajiangusha hovyo.

Silva ambaye ni beki aliyejiunga hivi karibuni na klabu ya Paris Saint-Germain, anaamini kwamba straika Neymar mwenye miaka 20 alichapwa sana kiatu na kunyimwa penati za wazi na anaamini kwamba ‘dogo’ huyo wa Santos sasa ameanza kuathiriwa na tuhuma kwamba huwa anajiangusha kirahisi.

"Hii ndio hofu yangu," Thiago Silva alikaririwa akisema na mtandao wa Globoespote. "Anafanyiwa madhambi lakini refa anaachia tu.

"Hata mashabiki waliguswa na faulo mbaya aliyochezewa Neymar ndani ya eneo la penati. Mimi nilikuwa mbali, lakini ilionekana kama jamaa alimshika shingo na kumvuta."

Katika mechi hiyo, Brazil walipata penati moja wakati wakishinda 2-0, huku Neymar akifunga penati hiyo baada ya Hulk kuangushwa na Micah Richards. Awali, kikosi cha Brazil kinachonolewa na kocha Mano Menezes kilipata bao la utangulizi kutokana na mpira wa kichwa uliopigwa na Sandro.

No comments:

Post a Comment