Saturday, July 21, 2012

ROBIN VAN PERSIE SASA AZIGONGANISHA RASMI MAN U, MAN CITY


Straika Robin Van Persie

MANCHESTER
HATIMAYE klabu mahasimu za Manchester City na Manchester United zimetuma maombi rasmi ya ya kumtwaa straika nyota aliyekataa kusaini mkataba wa Arsenal, Robin van Persie.

Gazeti la The Sun limesema leo kuwa Man City wametuma ofa ya paundi za England milioni 15 kwa Arsenal jana (bilioni 36) huku pia kocha wa Man U, Alex Ferguson akithibitisha kutuma ofa ya kumtwaa kwa paundi za England milioni 13 (Sh. Bilioni 32).

Hata hivyo, Arsenal wamekaririwa wakisema kuwa hawako tayari kumuachia nahodha wao huyo aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita kwa dau lisilofikia walau paundi za England milioni 20 (Sh. Bilioni 50)
Juventus pia wamejitosa katika vita ya kumuwania na tayari wameshatoa ofa ya kumtwaa kwa paundi za England milioni 8 (Sh. Bilioni 20).

Jana, Arsenal walisema kuwa wako radhi kumuachia ikiwa watapewa ofa sahihi itakayofikia dau wanalotaka.No comments:

Post a Comment