Saturday, July 21, 2012

TAZAMA DOGO ‘SHABIKI’ WA YANGA ALIVYOKUWA AKISHANGILIA KISTAILI BAADA YA KUIFUNGA APR

Hebu mcheki dogo... anashangilia kwa mtindo uleule wa akina  Felix Katongo wa Zambia, huku babu yake akimuunga mkono kwa kushangilia Yangaa...Yaanga! 
Waje wengine tuwakate shingo... ndivyo dogo anavyoonekana wakati akishangilia ushindi wa Yanga wa 2-0 dhidi ya APR katika Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.
Wacha weee....! Mcheki dogo na manjonjo yake. Yote hii ni utamu wa ushindi wa 2-0 dhidi ya APR jana.
Hapa yeye na babu yake wanaonekana kwa mbali baada ya kujichanganya na wanazi wengine wa Yanga waliokuwa wakishangilia mfululizo nje ya Uwanja wa wa Taifa baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ngumu ya 'maafande' APR ya Rwanda.
Mashabiki wengine wa Yanga pia hawakuacha vituko. Watazame... wamebeba bonge la sanamu na kulitaja jina la mwenyekiti wa mahasimu wao Simba, Aden Rage wakati wakishangilia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya APR katika Kombe la Kagame jana.
Rage huyoooo....! Ndivyo mashabiki hawa walivyokuwa wakiimba kiuchokozi dhidi ya watani zao wa jadi Simba, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya APR jana.
Dogo mmoja ambaye ni shabiki wa Yanga alikuwa kivutio kikubwa kutokana na staili yake ya kushangilia kama akina Chris Katongo wa Zambia baada ya klabu hiyo ya Wanajangwani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya APR ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Said Bahanuzi alifunga mabao yote ya Yanga katika kila kipindi na kuibua shangwe na nderemo za mashabiki wa Yanga ambao wengi walitoka uwanjani hapo kwa maandamano ya ngoma na nyimbo huku ‘dogo’ huyo akiwa kivutio, akishangilia kwa staili ya kujikata shingo kama walivyokuwa wakifanya wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia wakati wa michuano waliyokuja kuibuka mabingwa ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2012) zilizoandaliwa kwa pamoja na nchi za Gabon na Equatorial Guinea.

No comments:

Post a Comment