Lucas Moura |
Thiago Silva |
PARIS, Ufaransa
BEKI mpya wa PSG, Thiago
Silva hashangazwi kuona kuwa Manchester United wanahaha kumsajili mchezaji
nyota wa klabu ya Sao Paulo ya Brazil, Lucas Moura.
Silva ambaye ni nahodha wa
timu ya taifa ya Brazil itakayoshiriki michuano inayoanza wiki ijayo ya
Olimpiki jijini London na hivyo kuwa karibu na Moura kwenye kikosi chao cha
taifa, amemuelezea Moura kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu.
"Naona kuna kila dalili
kwa Lucas kucheza katika Ligi Kuu ya England," alisema Silva.
"Licha ya kuwa ni
mfupi, yeye ni ngangari na pia ana nguvu za kutosha. Ni vigumu sana kumzuia.
"Na kwa kawaida katika klabu ya Manchester,
wanacheza na mawinga wawili -- alitamba Cristiano Ronaldo na sasa ni zamu ya Nani.
Lucas ana sifa zote walizo nazo wakali hawa (Ronaldo na Nani)."
No comments:
Post a Comment