Saturday, July 21, 2012

RONALDO: MWANANGU NI 'HANDSOME' KAMA MIMI VILE!


Hapa Ronaldo na mwanawe wakiponda maraha ndani ya boti ya kifahari kwenye fukwe za Saint-Tropez nchini Ufaransa.

Mtoto wa Ronaldo akiwa amebebwa na mchumba wa baba yake (Irina Shayk) wakati wakiwa mapumzikoni nchini Thailand mwishoni mwa wiki.

Ronaldo na mwanawe wakiwa ndani ya boti ya kifahari kwenye fukwe za Saint-Tropez nchini Ufaransa.

Ronaldo na mwanawe ndani ya boti, kwenye fukwe za Saint-Tropez nchini Ufaransa.

Hapa dogo anaonekana vizuri zaidi wakati akiwa amebebwa na baba yake. Ni handsome eeh... sivyo?

Si mnamuona dogo mwenyewe? Mcheki hapo kwa kati, akifaidi kubebwa na baba yake ndani ya boti ya kifahari kwenye fukwe za Saint-Tropez, Ufaransa.

THAILAND
STRAIKA Cristiano Ronaldo wa klabu ya Real Madrid haishi mbwembwe na majisifu. Safari hii ametoa mpya kwa kusifu uzuri wa mtoto wake Cristiano Jr, akidai kwamba naye ni ‘handsome’ atakayekuwa na mvuto mkali kwa mademu kama alivyo yeye.

Ronaldo alimwagia sifa mtoto wake huyo aliyezaliwa mwaka 2010 wakati akizungumza katika mahojiano yake jana na kituo cha luninga cha Thai TV kilichopo nchini Thailand ambako Ronaldo, mtoto wake huyo na mchumba wake Irina Shayk walikuwa wakila bata kwa takriban wiki mbili za kuwa mapumzikoni.

"Ana nywele nzuri kama zangu, ni imara na zilizojisokota," Ronaldo alisema huku akitabasamu.
"Nalala na kuamka naye: mwanangu siku zote yupo pamoja na mimi."

No comments:

Post a Comment