Sunday, July 22, 2012

TFF YAWAPONGEZA VIONGOZI WAPYA SOKA DODOMA

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Julai 21 mwaka huu).

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema leo kuwa ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DOREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Dodoma.

Wambura alisena TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DOREFA chini ya uenyekiti wa Nasoro Kipenzi ambaye amechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.

Alisema uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Dodoma kwa kuzingatia katiba ya DOREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

"Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DOREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF," alisema Wambura.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika hoteli ya Dear Mama ni Nassoro Kipenzi (Mwenyekiti), Thadeo Kaliza (Makamu Mwenyekiti), Stewart Masima (Katibu Mkuu), Kepha Maswaga (Mhazini), Mulamu Ngh’ambi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Mohamed Aden (Mwakilishi wa Klabu TFF), Zawadi Kassim (Mjumbe Kamati ya Utendaji).

No comments:

Post a Comment