Sunday, July 22, 2012

RAMBIRAMBI MSIBA WA MTANGAZAJI JOSEPH MAPUNDA


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mtangazaji wa michezo wa Radio Wapo, Joseph Mapunda kilichotokea jana asubuhi (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, amesema leo kuwa msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Mapunda alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango wake wataukumbuka daima.
 

Wambura alisema TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Mapunda, Radio Wapo na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Mapunda mahali pema peponi. Amina


No comments:

Post a Comment