Sunday, July 29, 2012

SIKU ZA UCHUKUAJI FOMU VITAMBULISHO VYA TAIFA DAR ZAONGEZWA


Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu
Muda wa kujaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam sasa umeongezwa hadi Agosti 6, imefahamika.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa baada ya Agosti 6, hakutakuwa na siku nyingine zaidi zitakazoongezwa kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.

Taarifa hiyo imewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao hawajakwenda kwenye ofisi za mitaa yao ili kujaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa wafanye hivyo haraka, huku wageni wanaoishi nchini kihalali wakitakiwa vilevile kwenda kuchukua fomu namba mbili na kuzijaza ili kuomba vitambulisho hivyo.

Awali, zoezi la kujaza fomu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam lililoanza Julai 16 lilitakiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment