Sunday, July 29, 2012

CHICHARITO AKALIA KUTI KAVU MAN UTD

Chicharito (kulia) na Shinji Kagawa wakishiriki mazoezi ya Manchester United j\kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, Afrika Kusini Julai 17, 2012.

HATMA ya mshambuliaji Javier Hernandez 'Chicharito' klabuni Manchester United iko shakani.

Gazeti la Manchester Evening News limesema kuwa uwezekano wa kutua kwa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie – kama Sir Alex Ferguson atafanikiwa kuwapiku mahasimu wao Manchester City katika kumsajili Mholanzi huyo – utamsukuma Chicharito nje ya nafasi za kuanza Man United.

Huku Wayne Rooney na Danny Welbeck wakiwa tayari mbele ya Mmexico huyo katika machaguo ya kocha Fergie, pia kuwasili kwa Shinji Kagawa, ambaye atatumika nyuma ya mshambuliaji mkuu, itamfanya 'Chicharito' kuachwa mbali sana katika kugombea nafasi kikosini.

No comments:

Post a Comment