Tuesday, July 3, 2012

SERENA AMCHAPA BINGWA MTETEZI WIMBLEDON


Serena akionyesha vitu vyake kabla ya kumchapa Petra leo.

Chukua hiyo...! Serena akipiga mpira kimahesabu kabla ya kuibuka mshindi dhidi ya Petra na kutinga nusu fainali ya michuano ya Wimbledon leo.
LONDON, England
MATUMAINI ya Petra Kvitova wa Jamhuri ya Czech kutetea ubingwa wa michuano ya tenis ya Wimbledon yalizimwa jana na Mmarekani Serena Williams baada ya kuchapwa kwa pointi 6-3 7-5 katika mechi yao ya robo fainali leo.

Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na nyota hao kiliifanya mechi hiyo iwe na msisimko kama ya fainali.

Kwa ushindi huo, Serena sasa atacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa pambano jingine kali la robo fainali kati ya Victoria Azarenka wa Belarus na Tamira Paszek wa Austria.

No comments:

Post a Comment