Wednesday, July 4, 2012

VAN PERSIE ATABAKI KWA GHARAMA YOYOTE - WENGERKOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger atazungumza kwa njia ya simu na Robin van Persie wiki hii huku straika huyo akiendelea kudengulia ofa kubaki Emirates ya mkataba mpya wa miaka mitatu wenye mshahara wa paundi 130,000 (sawa na Sh. milioni 318) kwa wiki.

Lakini katika blog yake yake ya Eurosport, Wenger amesema: "Tunataka kumbakisha Robin van Persie kwa gharama yoyote, kwa sababu tunamtegemea yeye katika ushambuliaji."


Akiongeza presha kwa Mholanzi huyo, Wenger ameongeza: "daima nimekuwa nikimsapoti hata katika vipindi vigumu (vikiwemo vya kuwa majeruhi kwa muda mrefu), na natumai atamalizia soka lake akiwa Arsenal."


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yuko mapumzikoni baada ya Uhoalnzi kutolewa mapema katika michuano ya Euro 2012.


Wakati huo huo, mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amekanusha ripoti kwamba wameletewa ofa kwa ajili ya straika huyo.


Juventus walisemekana kuwasilisha ofa ya paundi milioni 8 kwa ajili ya nyota huyo, lakini Hill-Wood amesisitiza: "Kwa ninachofahamu hakuna yeyote aliyeleta ofa kwa ajili yake na yuko mapumzikoni hivyo hakuna mjadala.


"Hatuna mpango wowote wa kumuuza."


Manchester City, Barcelona na Real Madrid zote zimeripotiwa kumhitaji straika huyo.

No comments:

Post a Comment