Tuesday, July 3, 2012

AVB NI "KIMEO" SPURS ASEMA GLENN HODDLE



LONDON, England
GLENN Hoddle, kiungo wa Tottenham Hotspur, anaamini kwamba klabu yake ya zamani imecheza kamari kumteua Andre-Villas Boas kuwa kocha wao mpya.

Mreno huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya London kaskazini leo, akichukua nafasi ya Harry Redknapp aliyetimuliwa mwezi uliopita.

Ni ajira ya pili kwa Villas-Boas kwenye Ligi Kuu ya England baada ya utawala wake uliojaa matatizo katika klabu ya Chelsea kumalizika ndani ya miezi tisa tu. Alitimuliwa mwezi Machi kufuatia uvumi wa kutokuwepo kwa utulivu ndani ya chumba cha kuvalia.

Hoddle, ambaye aliichezea klabu hiyo kwa miaka 12 katika miaka ya 1970 na 80, na kurejea kama kocha mwanzoni mwa karne hii, alisema ameshangazwa na maamuzi ya mwenyekiti Daniel Levy kumpa ajira hiyo Villas-Boas.

"Sikutarajia kwamba Spurs ingefanya jambo hili," Hoddle aliiambia ESPN. "Ni zaidi ya kucheza kamari kwa sababu ya namna ambavyo mambo hayakwenda alipokuwa Chelsea.

"Nilidhani ingekuwa bora kwake kama angeenda kujijenga upya mahala kwingine kabla ya kurejea kwenye soka la Uingereza."

Gary Mabbutt, ambaye alicheza na Hoddle katika miaka 1980 na akacheza karibu mechi 500 katika kikosi cha Spurs, amesapoti Villas-Boas kurejesha heshima yake White Hart Lane.

"Ni kocha kijana, anataka kuwa bora hivyo amejifunza alipokuwa Chelsea," Mabbutt aliiambia Sky Sports.

"Tunataka kuwemo kwenye Ligi ya Klabu Bingwa kila mwaka. Tunaamini tuna kikosi cha vijana wadogo kilicho na uwezo huo."

No comments:

Post a Comment