Friday, July 20, 2012

SAID FELA WA TMK: JAMANI, SIO MIE NILIYEZAMA NA BOTI YA SKAGIT


Said Fela (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wasanii ewa Wanaume TMK.

Said Fela
MSANII Said Fela wa Kundi la Mkubwa na Wanawe na Meneja wa TMK Wanaume Family amewaondoa hofu mashabiki wake kwa kusema kuwa yeye hakuwemo katika boti iliyozama visiwani Zanzibar juzi.

Jina la Said Fela ni miongoni mwa yale yaliyojitokeza katika orodha ya watu 340 waliokuwamo katika boti iliyozama juzi ya Mv Skagit, kwenye eneo la Chumbe visiwani Zanzibar na majina hayo kuonekana leo katika mbao za matangazo za ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Ikiwa kuna jina kama langu, basi ni kwa sababu ya kufanana tu… mimi sikuwemo katika boti iliyozama ya Skagit na wala siku hiyo sikusafiri kwenda Zanzibar,” amesema Fela.

Baadhi ya watu wanaomjua Fela waliingiwa hofu juu ya uzima wake baada ya kuiona orodha hii hapa chini na kugundua lake likiwa miongoni mwa waliokuwamo kwenye boti ya Mv Skagit (jina la pili kutoka chini).

No comments:

Post a Comment