Friday, July 20, 2012

SERIKALI YAANZA KUZIKA MAITI WASIOTAMBULIWA KATIKA BOTI ILIYOZAMA YA SKAGIT


Mwili wa mtoto ukiwa mbioni kuzikwa leo. 
Kaburi likiwa tayari leo kuzikia mwili wa maiti inayoonekana ikiwa imeshavishwa sanda.
Wanajeshi wakisaidia shughuli ya kuzika miili hiyo visiwani Zanzibar leo.
Maiti mojawapo katika ajali ya boti iliyozama juzi ya Mv Skagit ikizikwa leo visiwani Zanzibar.
Askari wa vikosi mbalimbali wakiendelea leo kushirikiana na wananchi Zanzibar kuzika maiti zisizotambuliwa baada ya kuzama kwa boti ya Mv Skagit juzi.

ASKARI wa vikosi mbalimbali wanashirikiana na wananchi visiwani Zanzibar katika zoezi la kuzika miili ya watu walioshindwa kutambuliwa baada ya kufariki katika ajali ya kuzama kwa boti ya Mv Skagit juzi.

Aidha, shughuli za kusaka miili mingine zinaendelea kufanyika katika eneo la ajali, karibu na kisiwa cha Chumbe kisiwani Zanzibar  ambako boti hiyo ilizama wakati ikitokea jijini Dar es Salaam. 

Hata hivyo, uwezekano wa kunasua miili zaidi inayodaiwa kukwama ndani ya boti hiyo unaelezwa kuwa mdogo kwani chombo hicho kimezama chini kabisa na kufikia kina kinachokadiriwa kuwa mita 60 huku uwezo uliopo ni kufikia kina cha mita zisizozidi 30.

No comments:

Post a Comment