Ronaldo akichangia damu hospitalini |
Straika wa Real Madrid
na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameeleza sababu kubwa ya kutojichora ‘tattoo’
mwilini kama ilivyo kwa mastaa wengine wa soka kuwa ni kutokana na desturi yake ya kuchangia damu
mara kwa mara.
Ronaldo ameeleza hayo
kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambamo pia
aliambatanisha picha inayomuonyesha akitoa damu hospitalini.
“Sina tattoo mwilini kwa sababu huwa ninachangia damu
kila mara,” amesema Ronaldo.
No comments:
Post a Comment