Monday, July 23, 2012

MARADONA: RONALDO HAWEZI KUMFIKIA LIONEL MESSI


Messi akikokota mpira mbele ya kocha Diego Maradona.
Lionel Messi (kushoto) na Ronaldo wanavyoonekana katika mechi mojawapo ya La Liga kati ya Barcelona na Real Madrid.
Ni long taim kitambo... hapa Ronaldo (kushoto) akiwa na Messi wakati wa hafla ya kutangazwa kwa Mwanasoka Bora wa Mwaka 2008 wa FIFA. Ronaldo aliibuka kidedea na baada ya hapo, tuzo hiyo ikageuka kuwa mali ya Messi kwa miaka mitatu mfululizo. Mwaka huu itakuwaje? 
GWIJI wa Argentina, Diego Maradona amesema kuwa Straika Cristiano Ronaldo wa Real Madrid kamwe hatafikia mafanikio ya Muargentina mwenzake Lionel Messi wa klabu ya Barcelona.

Kuna mashabiki wengi wanaoamini kwamba Ronaldo alimfunika Messi msimu uliopita licha ya kwamba Muargentina huyo (Messi) aliongoza katika ‘ligi’ ya upachikaji mabao.

Lakini Maradona anasema: "Cristiano hatafikia hata siku moja mafanikio ambayo tayari Messi ameshayapata, ni kweli ana mashuti mazuri sana, lakini anahitaji kuwa na vitu vingine zaidi ya mashuti.
"Sitamzungumzia Messi kwa mabaya hata siku moja kwa sababu namjua… Messi anafunga magoli na kushangilia, Cristiano anafunga magoli na kusimama kama vile mtu anayeuza shampoo. Hiyo nd’o tofauti yao."

No comments:

Post a Comment