Thursday, July 19, 2012

PILIKA ZA UOKOAJI, KUTAMBUA MAITI ZAENDELEA

 Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya boti ya Mv Skagit iliyozama akiwa na simanzi ya kuondokewa na jamaa yake katika tukio la ajali hiyo baada ya kuutambua mwili wa jamaa yake katika viwanja vya Maisara.

Ndugu na jamaa wakiwa katika foleni kusubiri kutambua miili ya ndugu zao waliopata ajali ya kuzama kwa boti ya Kampuni ya SeaGull jana.
 
Wananchi wakiwa katika viwanja vya mpira vya Mairasa kusubiri kutambua miili ya jamaa zao.

 
Vijana wa Red Cross wakiwa katika bandari ya Malindu wakisubiri majeruhi na maiti wa ajali ya boti ya abiria.

Boti ya Kampuni ya Azam Marine ikiwasili katika bandari ya Malindi ikiwa na baadhi ya abiria waliookolewa

Kijana aliyeokolewa kutoka katika ajali akisaidiwa na askari
Kijana akibebwa baada ya kuokolewa

Manusura akiteremka kwenye boti ya uokaji







 Madakatari wa Hospitali Kuu ya Taifa ya Mnazi Mmoja wakitoa huduma kwa majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi.

Majeruhi  wa ajali ya Boti kutoka nje ya Nchi ambao ni watalii waliokuwa wakija Zanzibar kutembea kwa ajili ya Utalii wakiwasili katika hospital kuu ya Mnazi Mmoja kwa kupata huduma zaidi wakisaidiwa na wahudumu wa huspitali hiyo

Majeruhi  wa ajali ya Boti kutoka nje ya Nchi ambao ni watalii waliokuwa wakija Zanzibar kutembea kwa ajili ya Utalii wakiwasili katika hospital kuu ya Mnazi Mmoja kwa kupata huduma zaidi wakisaidiwa na wahudumu wa huspitali hiyo

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi, akizungumza na daktari bingwa wa kufanya uchunguzi wa maiti wa ajali kupitia uchunguzi wa kuchukua vinasaba DNA, Dk. Ahmed Makata, wakati alipotembelea eneo maalum la kuwekea miili ya maiti wa ajali ya boti katika viwanja Maisara.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Said Mwema (katikati) wakati alipofika katika viwanja vya Maisara kuangalia shughuli za utambuzi wa maiti zinavyoendelea jana usiku.CHANZO: http://othmanmapara.blogspot.com/ 

No comments:

Post a Comment