Friday, July 20, 2012

PATA MAJINA YA WATU 340 WALIOKUWAMO NDANI YA BOTI ILIYOZAMA JUZI YA SKAGIT


Vijana wa Kamanda Suleiman Kova nao walifika leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujaribu kutazama majina ya watu waliokuwamo katika boti iliyozama juzi ya Mv. Skagit. 

Harakati za kukagua majina ya watu waliokuwamo kwenye boti iliyozama ya Mv Skagit zikiendelea leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Vijana wa Kova wanaonekana wakiendelea kucheki kama kuna watu wanaowafahamu katika orodha ya watu waliokuwamo kwenye boti iliyozama ya MV Skagit katika mbao za matangazo za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo.

Hawa waliwahi mapema leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam  kuanza zoezi la kukagua majina ya watu waliozama na boti ya Mv Skagit juzi ili kujua kama kuna watu wanaowafahamu.

Wakazi mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza leo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa huo kutazama majina 340 ya watu waliozama na boti ya MV Skagit juzi ili kuona kama kuna ndugu zao.

Boti hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, ilizama mishale ya saa 7:00 mchana juzi baada ya kile kinachoelezwa kuwa ni kupigwa na wimbi kali kabla ya kupinduka wakati ikikatiza kwenye eneo la Chumbeni.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliokuwa wamefika kuangalia orodha hiyo leo wameelezea kusikitishwa kwao na uandishi wa majina hayo ambayo yameandikwa kwa mkono na kuwapa shida ya kusoma kwa uhakika. Wengine pia walishangaa kutokuta majina ya ndugu zao ambao wanadai kwa uhakika kuwa walikuwemo ndani ya boti hiyo. 

Ifuatayo ni sehemu ya majina ya watu 340 ambao orodha yao kutoka katika kampuni inayomiliki boti ya Skagit iitwayo Seagull Sea Transport Company Limited ilipelekwa serikalini na kubandikwa leo katika mbao za matangazo za ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili wananchi wapate nafasi ya kwenda kutazama na kujua kama kuna ndugu zao.

 No comments:

Post a Comment