Sunday, July 8, 2012

MURRAY ACHAPWA TENA FAINALI YA TENISI NA FEDERER

Roger Federer (kushoto) akishangilia ubingwa wa taji la tenisi la Wimbledon baada ya kumfunga Andy Murray wa Uingereza (wa pili kulia) baada ya mechi yao ya fainali leo.

Baba wa mcheza tenisi Roger Federer, ambaye pia anaitwa Roger Federer, mke wa Federer, Miloslava Vavrinec na binti zao Myla Rose na Charlene Riva wakishangilia ushindi baada ya Roger kumfunga Andy Murray na kutwaa taji la Wimbledon leo.

Roger Federer (kulia) akishangilia huku Andy Murray (kushoto) akiwa hoi.

Naweka marekodi tu hadi noma... Federer akishangilia ubingwa wa Wimbledon.

Wazee wa "vuvuleza" Waingereza tutaongelea wapi...? Andy Murray (kulia) akiwa na tuzo yake ya ngao ya mshindi wa pili baada ya kufungwa katika fainali na Roger Federer (kushoto).

JARIDIO la Muingereza Andy Murray kutwaa ubingwa tenisi wa Wimbledon lilizimwa na Roger Federer wakati Mswisi huyo alipotwaa taji lake la 17 la michuano mikubwa ya Grand Slam na kufikia rekodi ya kubeba mataji mengi makubwa iliyokuwa ikishikiliwa na Pete Sampras.


Murray (25) alikuwa akiwania kuwa Muingereza wa kwanza kutwaa taji la mchezaji mmoja mmoja tangu Fred Perry aliposhinda taji hilo mwaka 1936.


Lakini Federer mwenye umri wa miaka 30 alishinda kwa 4-6 7-5 6-3 6-4 na kurejea kuwa mcheza tenisi Na.1 duniani katika chati ya viwango vya ubora.


Murray aliyejawa na machozi baada ya mechi sasa amekuwa mchezaji wa kwanza kupoteza fainali zake za kwanza zote nne alizofikia.


Alikuwa Muingereza wa kwanza kucheza fainali ya Wimbledon tangu Bunny Austin alipofanya hivyo mwaka 1938, lakini alishindwa kutimiza ndoto zake.


"Kila mtu alikuwa akizungumzia presha ya kucheza fainali ya Wimbledon, lakini haikuwa hivyo kwa mashabiki waliokuwa wakishuhudia uwanjani - walinipa sapoti kubwa ya aina yake," alisema Murray huku akitokwa na machozi baada ya kipigo hicho.

No comments:

Post a Comment