Monday, July 9, 2012

KIKAPU NIGERIA WAFUZU OLIMPIKI, WAWAFUATA AKINA LEBRON JAMES, KOBE

Wachezaji wa timu ya taifa ya kikapu ya Nigeria wakishangilia baada ya kuwafunga Jamhuri ya Dominic wakati wa mechi yao ya FIBA ya kuwania kufuzu Olimpiki 2012  mjini Caracas jana. Nigeria wamefuzu kwa Olimpiki za 2012 za London. Picha: REUTERS

Mchezaji wa timu ya taifa ya kikapu ya Nigeria, Anthony Oludewa Skinn (kulia) akishangilia baada ya kuwafunga Jamhuri ya Dominic wakati wa mechi yao ya FIBA ya kuwania kufuzu Olimpiki 2012  mjini Caracas jana. Nigeria wamefuzu kwa Olimpiki za 2012 za London. Picha: REUTERS
Mchezaji wa timu ya taifa ya kikapu ya Nigeria, Anthony Oludewa Skinn (kulia) akishangilia baada ya kuwafunga Jamhuri ya Dominic wakati wa mechi yao ya FIBA ya kuwania kufuzu Olimpiki 2012  mjini Caracas jana. Nigeria wamefuzu kwa Olimpiki za 2012 za London. Picha: REUTERSCARACAS, Venezuela
TIMU ya taifa ya kikapu ya Nigeria itashiriki kwa kwanza kabisa katika historia ya michezo ya Olimpiki mjini London baada ya kuwafunga Jamhuri ya Dominic kwa pointi 88-73 katika mechi ya kuamua timu ya kufuzu jana Jumapili.


Wakiwa wamewasili nchini Venezuela kama timu isiyopewa nafasi katika michuano iliyohusisha timu 12 ya kuwania nafasi tatu za kufuzu Olimpiki ya London, Nigeria walikamilisha kampeni zao za kukumbukwa kwa ushindi mnono dhidi ya Dominicans - timu nyingine ambayo haikutarajiwa.


Mbali na taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo liliwashangaza mabingwa wa zamani wa Ulaya, Ugiriki, na kutinga nusu fainali, Russia na Lithuania pia zimefuzu kwenda Olimpiki London baada ya kushinda Jumamosi.


Timu hizo tatu zitaungana na Marekani, Argentina, Hispania, Ufaransa, Tunisia, Brazil, Australia na China ambao walifuzu mapema pamoja na wenyeji Great Britain.


Nyota wa Nigeria, Ike Diogu alifunika kwa rekodi nzuri binafsi akifunga pointi 25 na kuwahi ribaundi 10, akimfunika mpinzani wake wa Dominica, Al Horford wa timu ya kikapu ya NBA ya Atlanta Hawks aliyefunga pointi 12 huku 5 tu kati ya hizo akizifunga wakati wa mchezo, nyingine mitupo huru.

No comments:

Post a Comment