Sunday, July 29, 2012

MTAZAME LIONEL MESSI ANAVYOKULAGA BATA NA MREMBO WAKE ANTONELLA....... NI BALAAAAAA!

Pendedhaaa eeenh....! Messi na mpenzi wake aliye mjamzito kwa sasa, Antonella Roccuzzo, wakiwasili katika eneo la mnuso wa harusi ya Iniesta hivi karibuni.

Mshumu tena...! Messi na demu wake Antonella Roccuzzo wakijiachia ufukweni.

Messi na mepnzi wake Antonella Roccuzzo kwa mbwembwe nd'o wenyewe.... Eti hapa wanajifanya wamesusa!
Mnaangalia nini? Messi akiendelea kujiachia ufukweni na mpenziwe Antonella Roccuzzo 

Mmmhh... ni raha tupu. Hapa Messi na demu wake Antonella Roccuzzo wakiponda maraha ndani ya boti ya kifahari

Hapa Meesi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakiwa ndani ya boti ya kifahari

Ni kujiachia ufukweni kwa kwenda mbele.... hapa Messi na mpenzi wake Antonella sijui walikuwa Coco Beach?

Duh...ni fulu kujiachia. Hapa ni wakati Antonella akiwa mapumzikoni na Messi ndani ya boti ya kifahari, siku chache kabla hajashika ujauzito. 

Sijui turudi tena ndani ya boti? Hapa Messi na Antonella wakijianika juani baada ya kuogelea weee hadi wakatepeta kwa uchovu.

Sasa akaunti yetu ina mihela kibao... soka linalipa bwana. Kwanini tusitafute mtoto kama wa Cristiano Ronaldo? Pengine ndivyo Antonella na Messi wanavyoambiana wakati wakiendelea kula bata ufukweni.

Soma meseji hii... Messi na Antonella wake wakiendelea kuponda maraha baada ya msimu wa ligi kumalizika.
Messi sio tu anacheza soka, bali anapenda soka... hii ilikuwa mwezi uliopita wakati akijiachia kwenye fukwe za Miami, Marekani.

Messi akiwa na kibukta chake cha ufukweni wakati akiwa mapumzikoni Miami, Marekani.

Messi na washkaji zake wakifaidi maisha kwenye fukwe za Miami, Marekani mwezi uliopita

Messi na mpenzi wake Antonella wakikatiza mitaa. Hapa ni kabla Antonella hajashika ujauzito.

Sijui ntapata mtoto wa kiume kama Cristiano Ronaldo? Hapa Messi akisinzia baada ya kuchezea sana maji kwenye fukwe za Miami, Marekani mwezi uliopita.


Messi na demu wake Antonella wakikatiza katika mitaa ya ufukweni walikoenda kufaidi samaki-samaki.

Ya nini tabu wakati raha ziko tele duniani? Messi, demu wake Antonella na wapambe wakiendelea kujiachia ufukweni.
Messi, demu wake Antonella na wapambe zao wakianza safari ya kwenda kuvua samaki... ni raha juu ya utamu!

Huyu ndiye Antonella, kimwana anayemuondolea upweke Lionel Messina kumsaidia katika kutumia mabilioni ya fedha anayoingiza kila mwaka na kuwapita wanasoka wote duniani.

Twende mpenzi... Messi na demu wake Antonella wakiwa ufukweni.

Antonella akiwa katika pozi lake linalomtuliza Messi... hapa jini Messi hafurukuti, chenga zake, magoli yake ya kichawi na kasi yake ya umeme awapo uwanjani huishia hukooooo.... sio mbele ya  kimwana huyu ati!
Nani kasema Lionel Messi mpole? Basi ukimtaka ugomvi ni rahisi sana... mguse huyu kimwana wake Antonella. Kama hajakutoa manundu kachinje mende!

Mrembo Antonella Roccuzzo ndiye tulizo la roho la Lionel Messi, nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

Kwa muda mrefu sasa, Messi na Antonella wamekuwa wakiambatana kwenye viwanja vya kuponda maraha, wakihama kutoka fukwe moja na kwenda sehemu nyingine ya kujidai, hasa nyakati ambazo Messi huwa 'free' baada ya kumalizika kwa msimu wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Hivi sasa, penzi la wapendanao hawa limenoga kwelikweli na Messi alishatangaza tangu mwezi uliopita kwamba wako mbioni kupata mtoto wake wao wa kwanza.

"Najua atakuwa ni mtoto wa kike," alikaririwa Muargentina Messi, ambaye ni mshindi mara tatu mfululizo wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia.

"Sitaki kueleza zaidi kwa sababu huwa hatupendi kuzungumzia maisha yetu binafsi, lakini hilo limeshathibitika na kuleta furaha kwa familia yangu na familia yao (Antonella). Tunasubiri kwa hamu siku hiyo ya kupata mtoto," mchezaji huyo nyota wa Barcelona alikaririwa akisema.

No comments:

Post a Comment