Sunday, July 29, 2012

WILSHERE NJE HADI OKTOBA

Jack Wilshere
Arsenal wanayakosa sana haya mambo... Wilshere akiambaa na mpira
Jack Wilshere wa Arsenal akimfungisha tela Michael Carrick wa Manchester United wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Mei 1, 2011.
Jack Wilshere wa Arsenal Kevin akimtoka Kevin Devies wa Bolton wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Reebok mjini London, England Mei 1, 2011.
Jack Wilshere wa timu ya taifa ya England akisaidiwa kuinuka na mchezaji mwenzake Scott Parker (kushoto) huku John Terry akishuhudia wakati wa mechi yao ya Kundi G la kuwania kufuzu kwa fainali za UEFA Euro 2012 dhidi ya Uswisi kwenye Uwanja wa Wembley mjini London, England Juni 4, 2011.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wa klabu hiyo Jack Wilshere hataweza kucheza kabla ya Oktoba.

Kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 20 alikosa msimu wote wa 2011-12 kutokana na matatizo ya 'enka', na akafanyiwa pia upasuaji mdogo wa goti mwezi Mei

"Tunatumai, tutampata Wilshere uwanjani Oktoba," alisema Wenger, kuelekea mechi yao ya mwisho katika ziara yao ya barani Asia mjini Hong Kong leo.

"Kwa kwa Abou Diaby amerejea, itakuwa kama tumesajili wachezaji wapya wawili. Kikosi kitakuwa ngangari na cha ushindani."

Wilshere aliumia 'enka' yake ya mguu wa kulia Juni mwaka jana na akafanyiwa upasuaji uliofanikiwa, kabla ya kujitonesha wakati akipona Januari.

Majeraha ya muda mrefu ya goti yalimrejea wakati akiuguza enka, jambo lililomfanya akose Euro 2012.

Wilshere anatumai kuanza mazoezi mepesi Agosti, huku malengo yake yakiwa ni kurejea kikamilifu Oktoba.

Jambo hilo linamaanisha kwamba atakosa mechi mbili za timu yake ya taifa ya England za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Moldova na Ukraine, zitakazochezwa mapema Septemba.

No comments:

Post a Comment