Wednesday, July 25, 2012

MESSI AIGHARIMU BARCA

Lionel Messi

BERCELONA imepoteza euro 400,000 (sawa na Sh. milioni 755) kwa Hamburg kama sehemu ya maafikiano kwa ajili ya mechi yao ya kirafiki ya jana usiku.

Barca ilishinda 2-1 mechi hiyo - ambayo ilikuwa ni sehemu ya sherehe za kutimiza miaka 125 ya klabu hiyo Hamburg SV - bila ya Messi, ambaye alikosa kutokana na kuwa maajeruhi.

Kukosekana kwake kumeigharimu Barca euro 400,000 ambazo zilikuwemo katika kipengele cha maafikiano baina ya klabu hizo mbili kwamba mwanasoka bora huyo wa dunia ni lazima acheze, limesema gazeti la AS.

Barca watacheza mechi tano za kirafiki (nne barani Ulaya na moja Afrika) ambazo zitaiingizia klabu hiyo kubwa yenye matatizo ya kifedha euro milioni 6 (sawa na Sh. bilioni 11).

No comments:

Post a Comment