Wednesday, July 25, 2012

INZAGHI ASTAAFU, AJIUNGA NA BENCHI LA UFUNDI MILAN

Filippo Inzaghi akipungia mashabiki baada ya kucheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.

Mkurugenzi Mtendaji wa AC Milan, Adriano Galliani akimkumbatia Filippo Inzaghi baada ya kucheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.

Filippo Inzaghi akiwa na mwanae, Tomasso, baada ya kucheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.

Filippo Inzaghi akilia wakati akiaga mashabiki baada ya kucheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.

Filippo Inzaghi akishangilia goli lake alilofunga katika mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.

Filippo Inzaghi akifunga goli katika mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo iliyokuwa ya Serie A dhidi ya Novara Calcio kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan, Italia Mei 13, 2012.
ROME, Italia
FILIPPO Inzaghi ametangaza kustaafu soka jana Jumanne, na amesema atajiunga na benchi la ufundi la timu ya vijana ya AC Milan.

"Muda wangu na Milan umemalizika kwa namna nzuri iwezekanavyo, kwa mechi ya mwisho, hivyo ilikuwa poa sana," Inzaghi (38), aliviambia vyombo vya habari vya Italia.

"Hivi sasa nina ndoto nyingine, ambayo ni kuwa kocha na natumai kutwaa kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya."

Inzaghi, ambaye amefunga magoli 156 katika mechi 370 za Ligi Kuu ya Italia (Serie A), aliongeza: "Nisingeweza kwenda kucheza soka mahala kwingine, kwa sababu siwezi kuondoka Milan. Leo nimepata ofa kutoka England, lakini siwezi kuondoka Milan.

"Nimesaini mkataba wa miaka miwili na nitaifundisha timu ya vijana, kisha siku moja natumai nitaiongoza timu ya wakubwa pia."

No comments:

Post a Comment