Wednesday, July 25, 2012

MDOGO WA HAZARD NAYE RASMI ASAJILIWA CHELSEA

Thorgan Hazard akiwa katika jezi ya Lens (kushoto) na picha ndogo kaka yake Eden akishikilia jezi ya Chelsea baada ya kusajiliwa.

LONDON, Uingereza
CHELSEA imemsajili yosso wa klabu ya Lens, Thorgan Hazard ambaye anaungana na kaka yake Eden Hazard kwa mabingwa hao wa Ulaya, klabu hiyo ya Ligi kuu ya England ilisema  jana.

Thorgan, 19, ni mdogo kwa miaka miwili kwa kaka yake mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Eden, ambaye alisajili kujiunga na Chelsea akitokea Lille mwezi uliopita, na huenda akacheza katika eneo moja la kiungo cha ushambuliaji na kaka yake.

Alijiunga na Lens akiwa na umri wa miaka 14 na akapandishwa katika timu ya wakubwa msimu uliopita, ambao alicheza mechi 14 za Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) ikiwemo aliyoingia akitokea benchi ya ufunguzi wa msimu.

Thorgan ameichezea Ubelgiji katika timu za taifa za vijana wa umri mbalimbali na alikuwemo kwenye kikosi kilichocheza michuano ya Euro 2011 ya U-19.

Atajiunga na kikosi cha Chelsea cha U-21 kwa ajili ya kujiandaa na msimu huku kukiwa na mpango wa kutolewa kwa mkopo ili kumsaidia kuongeza ujuzi, klabu hiyo iliongeza katika tovuti yao (www.chelseafc.com).

Vijana hao wa Hazard, ambao wazazi wao walikuwa wanasoka, wpte walikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji huko Tubize na huenda akajumuika orodha ndefu ya wachezaji kutoka familia moja kuichezea klabu Chelsea wakiwemo Ray na Graham Wilkins, Ron na Allan Harris, John na Peter Sillett na Chris na William Ferguson.

No comments:

Post a Comment