Wednesday, July 25, 2012
ARSENAL YAKARIBIA KUMSAJILI CAZORLA
ARSENAL wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa timu ya taifa ya Hispania Santi Cazorla baada ya mkali huyo kuafiki malipo binafsi na klabu hiyo.
Kiungo huyo wa Malaga anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kutua London Kaskazini katika wiki chache zijazo, mwaka mmoja baada ya kutakiwa kwa mara ya kwanza na Arsene Wenger.
Arsenal imeweka mezani ada ya uhamisho ya paundi milioni 15.6 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wenye vipaji vikubwa katika La Liga na dili linatarajiwa kukamilika kutokana na dhamira ya mchezaji huyo kuhama.
Cazorla alijiunga na Malaga Juni mwaka jana akitokea Villarreal - ambao baadaye walishuka daraja - lakini amekuwa katika malumbano na klabu yake kutokana na kutolipwa mishahara yake.
Hali ya kifedha si njema katika klabu hiyo inayomilikiwa na Waarabu, ambayo inadawiwa kodi kubwa na serikali ya Hispania, pamoja na madeni kibao ambayo hayajalipwa kuhusiana na uhamisho wa wachezaji.
Na sasa gazeti la The Guardian limesema kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 atakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kutimka klabuni hapo ili kusaidia kulipa madeni.
Cazorla, ambaye alifunga 'frikiki' nne msimu uliopita, alicheza takribani katika kila katika kiungo na ushambuliaji, na itakuwa nyota wa tatu kutua Arsenal katika kipindi hiki cha usajili, baada ya Lukas Podolski na Olivier Giroud.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment