Nuri Sahin |
MANCHESTER United sasa wameelekeza macho yao kwa kiungo wa
Real Madrid, Nuri Sahin baada ya kuona wakikatishwa tama na mpango wao wa
kumnasa Mbrazili Lucas Moura.
Straika (kupitia mtandao wa Goal.com), inatambua kwamba Man U
wanasaka kiungo mwingine badala ya chipukizi Moura wa Sao Paulo, ambaye bei ya kumnunulia waliyotajiwa
na klabu yake ni euro milioni 38.3, na wamegusia kwamba Sahin ni ‘kifaa’
watakachokiata kwa bei poa baada ya nyota huyo kutambua ugumu wa kupata namba
katika kikosi cha mabingwa wa La Liga, Real Madrid.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uturuki amekuwa ni mchezaji wa ziada katika kikosi cha
Real tangu alipotua akitokea Borussia Dortmund msimu uliopita na kuandamwa na
majeraha na kucheza kwa kiwango cha chini.
Jose Mourinho anaweza kumhakikishia Sahin nafasi ya kutosha
ya kucheza katika mechi zao za maandalizi ya msimu ili kuona kama atafaa kuwemo
katika kikosi cha vigogo hao wa La Liga, lakini ni wazi kwamba Real watakuwa
tayari kusikiliza ofa kutoka kwa Man U.
Bayern Munich na Galatasaray zimekuwa pia zikihusishwa na usajili
wa Sahin katika wiki za hivi karibuni. Tottenham pia walituma ombi la kumtaka
ili atumike kubadilishana naye na kiungo wao Luka Modric anayetakiwa sana na
Real Madrid, lakini ‘wakala za uso’ baada ya Sahin mwenye miaka 23 kukataa kutumika
kama chambo.
Sahin amesisitiza kuwa anataka kubaki Real Madrid msimu ujao
ili apiganie namba katika kikosi cha kwanza, akisema: "Nina usongo wa
kupata mafanikio hapa na ninataka kuthibitisha thamani yangu kwa Real Madrid. Nina
ndoto za kutimiza katika klabu hii."
No comments:
Post a Comment