Romelu Lukaku |
LONDON, Chelsea
STRAIKA wa Chelsea Romelu Lukaku yuko katika hatua za
mwisho kusajiliwa kwa mkopo na klabu ya Fulham, imefahamika.
Mahasimu hao wa wa Jiji la London wako katika
hatua nzuri ya mazungumzo kuhusiana na mpango huo ambao utamfanya Lukaku achepukie
upande mwingine wa mji kwa mkataba mrefu wa mkopo.
Martin Jol ameruhusu uhamisho wa yosso huyo wa Mbelgiji baada
ya Chelsea kusema wazi kwamba ilikuwa ikiangalia uwezekano wa kuwatema, ama kwa
kuwauza kwa mkopo au kuwauza jumla baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha
kwanza.
Chelsea hawana kikwazo katika kumruhusu Lukaku, 19, kwenda
Fulham ikiwa atahakikishiwa nafasi zaidi za kucheza kulinganisha na ile aliyo
naso sasa Stamford Bridge.
Lukaku amezungumzia kutofurahishwa kwake na hali ya kutopewa
nafasi ya kutosha ya kucheza katika kikosi cha kwanza tangu asajiliwe na
Chelsea mwanzoni mwa msimu uliopita kwa dau la paundi za England milioni 18 akitokea Anderlecht.
Alisema kuwa “ameksirishwa sana” kuona kuwa ameanzishwa katika
mechi moja tu ya Ligi Kuu ya England na kudai kwamba hakutendewa haki na kocha
wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas.
Licha ya kuondoka kwa Didier Drogba na Salomon Kalou katika
kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi
na Nicolas Anelka aliyeondoka Januari, Lukaku bado hana uhakika wa kucheza
mbele ya mastraika Fernando Torres na Daniel Sturridge.
Chelsea na Fulham wameshakubaliana katika mambo ya msingi ya uhamishjo
wake wa mkopo, ambao unaweza kufanana kwa kiasi kikubwa na wa Gael Kakuta
katika mzunguko wa pili wa msimu wa 2010-11, wakati mshahara wa yosso huyo Mfaransa
ulipochangiwa kwa kiwango sawa na klabu hizo mbili.
Kama uhamisho huo utakamilishwa, Lukaku atakuwa ni
mshambuliaji wa tatu kusajiliwa na Fulham katika dirisha hili la usajili.
Klabu hiyo ya magharibi mwa London tayari imeshawasajili
Mladen Petric na Hugo Rodallega waliokuwa huru, kutoka katika klabu za Hamburg na
Wigan Athletic, lakini ikamuuza Andy Johnson kwa QPR na pia kushindwa katika mchuano
wake dhidi ya Reading kumuwania Mrusi Pavel Pogrebnyak, nyota wao waliyemtwaa
kwa mkopo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment