Luka Modric |
Mwenyekiti wa
klabu ya Tottenham inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Daniel Levy amestushwa na uamuzi
wa kiungo wao Luka Modric aliyekataa kusaini mkataba mpya uliomboreshea mshahara
wake mara mbili ili aichezee Real Madrid inayoshikilia ubingwa wa La Liga, Ligi
Kuu ya Hispania.
Modric, kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya Croatian, amekataa kusaini mkataba mpya wa
kumbakiza Tottenham, ambao ungemfanya awe mchezaji anayelipwa fedha nyingi
zaidi katika historia ya klabu hiyo ya jiji la London.
Real wamempa
Modric ofa ya kumlipa mshahara wa Euro milioni 4.5 kwa mwaka (Sh. bilioni 8.5),
wakati mkataba waliomuandalia Tottenham ili abaki unamhakikishia mshahara mnono
wa Euro milioni 5.4 kwa mwaka (Sh. bilioni 10).
Kwa kumaliza
kileleni mwa La Liga msimu uliopita, Real Madrid watashiriki Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya wakati Tottenham watashiriki michuano midogo ya Ligi ya Europa baada
ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini
wakipokwa nafasi ya kushiriki klabu bingwa Ulaya kwavile Chelsea iliyomaliza
nje ya ‘top 4’ ilitwaa ubingwa wa Ulaya na hivyo imejihakikishia nafasi ya
kutetea taji hilo.
No comments:
Post a Comment