Tuesday, July 24, 2012

KESI YA LULU YAPIGWA KALENDA TENA


Lulu akiwa katikati ya askari mahakamani.


Lulu akiwa na Kanumba katika picha hii iliyochukuliwa kutoka katika filamu.

MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeendelea kupiga kalenda kesi ya maombi ya kuchunguza utata wa umri halisi wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael (18) ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) hadi Agosti 20, mwaka huu.

Kesi hiyo ilitajwa jana na Msajili wa mahakama hiyo, Amir Msumi baada ya Jaji Dk. Fauz Twaib kuwa na udhuru wa kikazi.

Pande zote mbili hazikuwa na pingamizi la kuahirishwa kesi hiyo kutokana na kusubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufani kuhusu maombi yaliyowasilishwa na Upande wa Jamhuri wakiitaka mahakama hiyo kufanya mapitio ya uamuzi wa wa Jaji Dk. Twaib kukubali kusikiliza maombi hayo.

Awali upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani ukitaka ifanye mapitio ya kesi hiyo kuhusu uamuzi uliotolewa na Jaji Dk. Twaib kukubali kusikiliza maombi ya Lulu.

Mapema mahakamani hapo pande zote mbili ziliamriwa kuwasilisha vielelezo dhidi maombi hayo ambapo baada ya hatua hiyo, upande wa Jamhuri ulipeleka maombi Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Jaji Dk. Twaib kuesikiliza maombi hayo.

Katika maombi hayo, Mshtakiwa anadai kuwa umri wake ni miaka (17 )na sio miaka (18) kama ilivyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ambapo ameomba mahakama kuu kuchunguza utata huo na kuyatolewa maamuzi maombi yake.

Upande wa Jamhuri unawakilishwa na Mawakili wa Serikali Shadrack Kimaro akisaidiana na Elizabeth Kaganda huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Mawakili wa utetezi Florensi Massawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama.

Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba.


No comments:

Post a Comment