Thursday, July 5, 2012

IVORY COAST, SENEGAL ZAKUTANA KUWANIA KUFUZU AFCON 2013, KINA OKWI MIDOMONI MWA ZAMBIAJOHANNESBURG, Afrika Kusini
Ratiba ya raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu kwa fainali za zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2013) imetolewa usiku huu ambapo kutakuwa na mechi za nyumbani na ugenini na washindi wa jumla katika kila mechi ndio watakaoungana na wenyeji Afrika Kusini katika kinyang’anyiro kitakachoanza Januari mwakani.
Vigogo Ivory Coast na Senegal ambao waliambulia patupu katika fainali zilizopita (AFCON 2012) licha ya kutabiriwa awali kuwa ndio watakaobeba taji hilo, wamepangwa pamoja huku mabingwa watetezi, Zambia wakikumbana na akina Emmanuel Okwi wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.
Mechi hizo zimepangwa kama ifuatavyo:
 Mali v Botswana
 Zimbabwe v Angola
 Ghana v Malawi
 Liberia v Nigeria
 Zambia v Uganda
 Cape Verde v Cameroon
 Mozambique v Morocco
 Sierra Leone v Tunisia
 Guinea v Niger
 Sudan v Ethiopia
 Libya v Algeria
 Ivory Coast v Senegal
 DR Congo v Eq. Guinea
 Gabon v Togo
Jamhuri ya Afrika ya Kati v Burkina Faso
   Mechi za awali zitaanza kuchezwa kati ya Septemba 7-9 huku marudiano yakiwa kati ya Oktoba 12-14.

No comments:

Post a Comment