Nawanukuu wanaojua wawe kikosi cha kwanza... kocha mpya Tom akifanya mambo yake. |
Niyonzima, Shamte, Yondani, Taita.... tunapasha tu. Mambo ya leo hayo wakati wa mazoezi yao |
Sisi tunaogopa 'fri-kiki' za kubutuana machoni.... Wachezaji wa Shein Rangers wakiweka ukuta wakati Rashid Gumbo akipiga 'fri-kiki' iliyokwenda wavuni baada ya kugonga nguzo. Picha: Sanula Athanas |
Na Sanula Athanas
KOCHA mpya wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amesema kwa sasa hauangalii upinzani ulipo kati ya klabu yake
na klabu ya Simba kwa sababu ana jukumu la kuhakikisha anatetea Kombe la
Kagame.
Kocha huyo aliyasema hayo leo
asubuhi wakati wa mazoezi ya timu yake kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama
jijini Dar es Salaam.
Saintfiet alisema anaelewa vizuri
upinzani mkubwa uliopo kati ya klabu hizo nchini lakini aliweka wazi kuwa
hayuko tayari kuifundisha Yanga kwa kuangalia mtindo ama mwenendo wa mahasimu
wao, Simba.
“Nazijua vizuri sana Yanga na Simba
na mambo yote yanayozihusu klabu hizi, lakini nimekuja kuing’arisha Yanga.
Nimekuja kuinoa Yanga na jukumu kubwa nililonalo kwa sasa ni kuhakikisha
inanyakua Kombe la Kagame,” alisema Saintfiet.
“Nimeiangalia timu yangu
kwenye mazoezi, ina wachezaji wazuri. Nilipoambiwa wameshafanya usajili
niliingiwa na hofu labda wamesajili wachezaji dhaifu lakini nimeona kuna
wachezaji wazuri sana.”
Kocha huyo ameeleza pia kufurahishwa
na ukarimu wa Watanzania kwa mapokezi ambayo walimfanyia kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment