Monday, July 23, 2012

FERGIE: TUNAMTAKA MOURA, HATUJAAFIKIANA BEI BADO

Lucas Moura

Lucas Moura

Shuhudia maujuzi... Lucas Moura akifanya mambo

Sir Alex Ferguson... Hatujalala, wakali zaidi wanakuja Man U

KOCHA Sir Alex Ferguson amethbitisha kuwa Manchester United inataka kumsajili yosso wa kimataifa wa Brazil, Lucas Moura (19), lakini amekanusha ripoti zilizozagaa leo kwamba wameafikiana bei ya paundi milioni 26.

"Hatujaafikiana bei ya mchezaji. Tumeonyesha nia lakini hadi wakati huo tutakapokamilisha maafikiano, kwa sasa hatuwezi kusema ni mchezaji wetu."

Moura yumo katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki na amezivutia klabu nyingine kadhaa za Ligi Kuu, ikiwamo Chelsea, pamoja na Real Madrid na Inter Milan.

Ferguson tayari amewasajili wachezaji wawili, kiungo Mjapan Shinji Kagawa na Nick Powell kutoka Crewe, tangu Manchester City ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya mabao dhidi ya Man United.

"Kwa wakati huu tunaangalia machaguo mengine katika suala la kuleta wachezaji wapya," Ferguson aliongeza katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Shanghai, China, ambako Man U wako ziarani kujiandaa na msimu wa 2012-13.

"Hatujalala chali bila ya kufanya chochote. Tunajaribu kwa nguvu zote kuleta wachezaji wengine."

Vidic (30), amerejea mazoezini baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti na kulikuwa na matumaini kwamba nahodha huyo angecheza mechi ya ufunguzi wa ligi kwenye Uwanja wa Goodison Park dhidi ya Everton.

Lakini Ferguson amesema Evans, ambaye alifanyiwa upasuaji wa mguu ambao ulimweka nje ya uwanja mwisho wa msimu uliopita, huenda pia akakosa mwanzo wa msimu.

"Hamna uhakika wa asilimia 100 kwamba Jonny Evans na Vida watakosa mwanzo wa msimu," alisema.

"Jonny ataanza kukimbia leo (Jumatatu). Vida na Phil Jones wameanza mazoezi kamili leo, jambo ambalo linaleta matumaini.

"Kama nitamweka Rio Ferdinand katika hali ya uzima, basi Vidic na Jones watatupa ulinzi wa kutosha."

No comments:

Post a Comment