Monday, July 23, 2012

DROGBA AANZA KUONYESHA 'MAVITUZ' CHINA


Safiii... kweli Drogba unatisha! Drogba akipongezwa na wachezaji wenzake wa Shanghai Shenhua baada ya kutoa pasi kali ya bao lao la kusawazisha dhidi ya Guangzhou.
SHANGHAI, China
STRAIKA Didier Drogba amesema kuwa amefurahi kuona kuwa "kila kitu kilikwenda vizuri" katika mechi ya kwanza kuichezea klabu yake mpya ya Shanghai Shenhua baada ya kuingia akitokea benchi na kuisaidia kupata sare ya ugenini ya 1-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya China dhidi ya Guangzhou R&F jana.


Wakati timu yake ikiwa nyuma, Drogba aliingia uwanjani na kuiongezea nguvu Shenhua, akibadili hali ya mchezo kabla ya kutoa pasi kali kwa Cao Yunding aliyeitumia vyema kwa kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 68.


"Nimefurahi kwamba kila kitu kilikwenda vizuri katika dakika zangu 45 za kwanza tangu nitue hapa," Drogba aliwaambia waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.


"Mwanzoni ilikuwa ngumu kiasi kuendana na mchezo, lakini nilipozoea hali, nikaanza kufurahia mchezo.
"Sasa najihisi vizuri na kuzoea kila kitu nchini China. Ni raha tupu kucheza pamoja na mchezaji mwenzangu wa zamani, Nicolas (Anelka)."


Wakati huohuo, straika wa wapinzani wao, Yakubu Aiyegbeni alisema kwamba Drogba anaweza kuibeba Shenhua, ambayo hivi sasa inasuasua katika nafasi ya 12, na kuipa ubingwa kutokana na kiwango alichoonyesha katika mechi yake ya kwanza juzi.


"Leo (jana) alionyesha kiwango cha juu, aliongeza hali ya kujiamini ndani ya kikosi chao, unaweza kuona namna alivyocheza, wakati atakapokuwa fiti kwa asilimia 100, anaweza kuisaidia Shanghai kutwaa ubingwa wa ligi," alisema Yakubu.

No comments:

Post a Comment