Sunday, July 29, 2012

BARCA: TUNAMTAKA NEYMAR BAADA YA OLIMPIKI

Neymar

Neymar wa Brazil akiwania mpira dhidi ya Joe Allen wa timu ya Great Britain wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England Julai 20, 2012.
Neymar akifanya mambo yake...

Neymar wa Brazil akishangilia kufunga penalti dhidi ya timu ya Great Britain wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough, England Julai 20, 2012.

MAKAMU wa rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu ametangaza kuwa klabu hiyo inataka kumsajili nyota wa Santos, Neymar katika kipindi hiki cha usajili.

Bartomeu amebainisha kuwa wanayo matumaini ya kumpata mshambuliaji huyo mwenye kipaji wa Brazil baada ya fainali za Olimpiki zinazoendelea London.

"Sote tungependa Neymar aje hapa baada ya Olimpiki," Bartomeu aliripotiwa kuwaambia mashabiki wa Barca nchini Morocco ambako usiku wa jana Barcelona ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Raja Casablanca ya huko.

"Yeye ni mchezaji wa Santos (kwa sasa) lakini nina hakika Neymar atakuja Ulaya baadaye, na wakati huo utakapowadia tutakuwa makini ili ajiunge na Barcelona."

No comments:

Post a Comment