Saturday, July 7, 2012

CASILLAS APEWE TUZO BALLON d'Or - DE GEA

Iker Casillas

David de Gea - Man United

KIPA wa Manchester United, David de Gea anaona kwamba kipa chaguo la kwanza wa Real Madrid, Iker Casillas, anapaswa kupewa tuzo ya Ballon d'Or ya mwanasoka bora wa dunia.

Jarida la France Football lililoianzisha tuzo huyo kabla ya kuiachia kwa FIFA hivi karibuni, liliandika jambo hilo katika maoni ya mhariri.

Na De Gea aliliambia gazeti la AS: "Casillas ndiye kipa bora zaidi duniani.

"Amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu kwa miaka mingi na ndiye nahodha wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania.

"Ameshinda mataji matatu makubwa ya kimataifa (Kombe la Dunia na Ubingwa wa Euro mara mbili) katika miaka minne iliyopita, amekuwa sehemu ya soka la ushinda kwa miaka mingi.

"Wakati umefika sasa kutoa tuzo ya Ballon d'Or kwa golikipa. Iker anastahili."

No comments:

Post a Comment