ALIINGIA MADARAKANI AKITOKEA UPINZANI 2009
Hayati Atta Mills enzi za uhai wake. |
ACCRA, Ghana
Rais wa Ghana, John Atta Mills,
aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya koo, amefariki dunia katika jiji
kuu la nchi hiyo, Accra.
Taarifa kutoka katika ofisi yake yake
zilieleza kuwa rais huyo mwenye miaka 68 alikufa saa chache tu baada ya
kuzidiwa, lakini hakukuwa na maelezo zaidi.
"Kwa huzuni kubwa... tunatangaza
juu ya kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha rais wa Jamhuri ya Ghana,"
taarifa hiyo ilisema.
Atta Mills ameliongoza taifa hilo la
magharibi mwa Afrika tangu mwaka 2009 wakati chama chake kilichokuwa cha
upinzani kiliposhinda katika uchaguzi mkuu wan chi hiyo.
Msaidizi wa rais amesema kwamba Atta
Mills alilalamika kusumbuliwa na maumivu jana jioni na akafa leo mchana,
shirika la habari la Reuters liliripoti.
Alirejea Ghana baada ya kutoka
Marekani alikokwenda kuchunguzwa afya yake.
No comments:
Post a Comment