Monday, July 2, 2012

BALOTELLI ATARAJIA MTOTO

Balotelli akiwa na Raffaella

Balotelli akiwa na Raffaella

ROME, Italia
STRAIKA wa timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli alifahamishwa kwamba anatarajia mtoto wake wa kwanza saa chache kabla ya kufunga magoli mawili dhidi ya Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya Euro 2012, vyombo vya habari vya Italia vimeripoti leo.

Rafiki wa kike wa mchezaji huyo wa Manchester City, Raffaella Fico aliliambia jarida la udaku la Chi: "Nilimpigia simu Mario wakati akiwa na timu ya taifa kabla ya mechi dhidi ya Ujerumani na nikamwambia: 'unakumbuka ndoto yetu ya kuwa wazazi? Sawa. Ile ndoto imekuwa kweli. Natarajia mtoto. Mtoto wako'.

"Alibaki kimya kwanza, kisha akasema: 'umenipa habari nzuri kuliko zote duniani', aliniambia. Kisha siku iliyofuata uwanjani alifunga magoli mawili," Fico alikaririwa akisema.

Baada ya kuifunga Ujerumani 2-1, Italia ililala 4-0 kwa Hispania katika fainali mjini Ukraine jana Jumapili.

No comments:

Post a Comment