Kutoka kushoto ni Gerard Pique,
Pepe Reina, Fernando Llorente, Iker Casillas na Xavi Hernandez wakishangilia kombe
walilotwaa baada ya kuinyoa Italia 4-0 jana.
|
KIEV, Ukraine
IFUATAYO ni orodha ya rekodi
mbalimbali za kukumbukwa baada ya Hispania kuifunga Italia mabao 4-0 katika
mechi yao ya fainali ya Euro 2012.
* Hispania wamekuwa timu ya
kwanza kutwaa mara mbili mfululizo taji la Ulaya huku pia wakiwa mabingwa wa
Kombe la Dunia. Taji hilo la Euro lilikuwa la tatu kwa Hispania, hivyo kufikia
rekodi ya Ujerumani ambayo pia imewahi kubeba kombe hilo mara tatu.
* Ushindi wa tofauti ya mabao manne
ulikuwa ndio mkubwa kuliko yote katika historia ya fainali za Ulaya na pia
Kombe la Dunia.
* Vicente Del Bosque ni kocha wa
pili tu aliyewahi kutwaa kwa mpigo mataji ya Euro na Kombe la Dunia, akiungana
na Helmut Schoen, aliyeiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa ubingwa wa Ulaya
mwaka 1972 na kubeba Kombe la Dunia miaka miwili baadaye.
* Ushindi wa juzi wa Hispania
ulikuwa ndio wa kwanza dhidi ya Italia katika kwa miaka nane katika mechi za
michuano mikubwa (walishinda kwa penati baada ya sare ya 0-0 katika robo
fainali ya Euro 2008)
* Straika Fernando Torres amekuwa
mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali mbili za michuano ya Euro na kutwaa
kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora wa Euro 2012, akibebwa na pasi yake ya
bao na pia kucheza kwa dakika chache zaidi ya Mario Gomez ambaye pia
aliufikisha mabao matatu.
* Hispania hawajawahi kufungwa
katika mechi 12 zilizopita za fainali ya Euro na pia hawakuruhusu goli
katika mechi zao tano zilizopita, takwimu zote hizo zikiwa ni rekodi ya
michuano hiyo. Hawajawahi kufungwa katika mechi zao 10 za mtoano kwenye fainali
za Euro na Kombe la Dunia.
* Kipigo chao cha mwisho katika
mechi ya fainali za Euro kilikuwa ni cha 2-0 kutoka kwa Sweden wakati wa
kuwania kufuzu fainali za mwaka 2006, wakati huo ikiwa ni baada ya kucheza
mechi 29 mfululizo bila kufungwa.
* Mara ya mwisho Hispania
kufungwa baada ya kuongoza kwa bao 1-0 walilala kwa mabao 3-2 kutoka kwa
Ireland ya Kaskazini, Septemba mwaka 2006.
* Juzi ilikuwa ni mara ya tatu
kwa timu kuongoza kwa 2-0 kabla ya mapumziko katika mechi ya fainali ya Euro.
Italia iliifunga Yugoslavia 2-0 mwaka 1968 na Czechoslovakia waliichapa
Ujerumani Magharibi kwa penati mwaka 1976 baada ya kuongoza 2-1 hadi kufikia
mapumziko.
* Kipa wa Hispania, Iker Casillas
amekuwa mchezaji wa pili tu, pamoja na gwiji wa Ujerumani Franz Beckenbauer
(1972-1976) kuwa nahodha wa timu ya taifa aliyeiongoza nchi yake katika fainali
tatu za Euro/Kombe la Dunia.
* Casillas pia ni mchezaji wa
kwanza kushinda mechi 100 za kimataifa na pia ana rekodi ya kutofungwa katika
mechi 79 kati ya 136 alizoichezea timu yake ya taifa.
* Kiungo wa Hispania, David Silva
alihusika moja kwa moja katika mabao matano ya Euro 2012 (akifunga magoli 2, akitoa
pasi 3 za mabao), idadi ambayo ni kubwa kuliko wachezaji wote.
* Kipa Gianluigi Buffon wa Italia
alivunja rekodi ya Dino Zoff ya kucheza mechi nyingi za fainali za Euro/Kombe
la Dunia baada ya kucheza mechi ya 25 juzi. Ni Paolo Maldini (mechi 36) na
Fabio Cannavaro (mechi 26) ndio wanaompita kwa idadi ya mechi alizoichezea
Italia.
No comments:
Post a Comment