Wednesday, June 20, 2012

WATANZANIA MAMBO MAGUMU TUSKER PROJECT FAME

Mshiriki wa Tanzania katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Tusker Project Fame 5 (TPF5), Damian Mihayo (kulia), akiwa amesimama pamoja na mtangazaji wa jukwaani wa shoo hiyo ya televisheni Dkt. Mitch Engwang wakati wa shindano hilo. Mtanzania huyo ameingia katika ukanda wa hatari wa kupigiwa kura ya kutoka. Mwenzake Imani Lissu, ambaye pia aliwahi kuwa mshiriki wa shindano la Bongo Star Search, tayari ameshaaga kambi ya mashindano ya TPF5 iliyopo nchini Kenya.

Mshiriki wa Tanzania katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Tusker Project Fame, Imani Lissu, ambaye pia aliwahi kuwa mshiriki wa shindano la Bongo Star Search, akiimba wakati wa shindano TPF Season 5 nchini Kenya. Kimwana huyo tayari ameshatolewa katika mashindano ya TPF5.

No comments:

Post a Comment