Wednesday, June 20, 2012

DROGBA AJIUNGA RASMI NA SHANGHAI SHENHUA

Didier Drogba akibeba kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wakati alipovaa jezi ya Chelsea kwa mara ya mwisho katika ushindi dhidi ya Bayern Munich kwenye Uwanja wa Fussball (Allianz) Arena Mei 19, 2012.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amejiunga na klabu ya China ya Shanghai Shenhua.


Didier Drogba amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu hiyo ya ligi kuu ya China.
Nyota huyo wa Ivory Coast atapaa kujiunga na timu yake mpya mwezi Julai.


Alisema: "Nimetafakari ofa zote nilizopata katika wiki chache zilizopita, lakini nimeona kwamba Shanghai Shenhua ndio mahala sahihi kwangu kwa wakati huu."


Kwa mara ya mwisho kwa mshambuliaji huyo kuvaa jezi ya Chelsea ni wakati alipofunga penalti ya ushindi na kutwaa kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwezi Mei.


Drogba sasa ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani Chelsea, Nicolas Anelka katika klabu hiyo ya China.

No comments:

Post a Comment