Saturday, June 16, 2012

Walcott: Asifu goli la kisigino la Welbeck

Theo Walcott wa timu ya taifa ya England (kushoto) akimpongeza Danny Welbeck kwa goli la tatu alilofunga wakati wa mechi yao ya Kundi D la Euro 2012 dhidi ya Sweden kwenye Uwanja wa Olympic mjini Kiev, Ukraine Juni 15, 2012 .

Theo Walcott wa timu ya taifa ya England (kulia) akimpongeza Danny Welbeck kwa goli la tatu alilofunga wakati wa mechi yao ya Kundi D la Euro 2012 dhidi ya Sweden kwenye Uwanja wa Olympic mjini Kiev, Ukraine Juni 15, 2012 .

Danny Welbeck wa timu ya taifa ya England (kushoto) akimliwaza Theo Walcott baada ya kuumia mchezoni wakati wa mechi yao ya Kundi D la Euro 2012 dhidi ya Sweden kwenye Uwanja wa Olympic mjini Kiev, Ukraine Juni 15, 2012.

KIEV, Ukraine
NYOTA wa Arsenal, Theo Walcott amemsifu mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck kwa kufunga goli kali la kisigino lililowapa England ushindi wa 3-2 dhidi ya Sweden katika mechi yao ya Euro 2012 mjini Kiev, Ukraine.
Walcott aliliambia gazeti la The Sun: "Danny ana ubora wa juu na nina hakika kuna mengi yanakuja kutoka kwake.
"Kama kuna watu hawajawahi kumsikia Danny katika michuano hii, watamfahamu sasa. Goli lile lina ubora wa juu. Nafasi ilikuwa ngumu na Danny akafanya ionekane rahisi.
"Lilikuwa ni bonge la goli, bila ya shaka ni moja ya magoli bora ya michuano hii — na sisemi hivyo kwa sababu ni rafiki yangu.
"Imeonyesha kwamba licha ya kuwa na umri mdogo anaweza kufanya mambo makubwa. Danny anaweza kufunga magoli. Si yeye tu, na Andy, pia.
"Tunao wachezaji wanaoweza kuingia kutokea benchi na kuleta mchango mkubwa katika kikosi hiki."
Walcott aliingia akitokea benchi na akabadilisha matokeo ambayo walikuwa nyuma 2-1 baada ya kufunga goli moja na kutoa pasi ya goli hilo kali la kisigino la Welbeck.
"Nina hakika Wayne Rooney atapata nafasi ya kuonyesha vitu vyake na atataka kujazia kile ambacho watu waliki-miss, atataka kuwapoza wachezaji wenzake wote, yeye ni mchezaji wa kiwango cha dunia ni ngumu kuacha nje lakini hayo ni maamuzi ya kocha. Tutaona kitakachotokea."

No comments:

Post a Comment