Saturday, June 16, 2012

Barcelona ni lazima isajili mabeki - Vilanova

Kocha mpya wa Barcelona, Tito Vilanova (kushoto) akiwa na kocha Pep Guardiola wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Uwanja wa Vicente Calderon Mei 25, 2012 mjini Madrid, Hispania. Mechi hiyo ilikuwa ya mwisho chini ya Guardiola, ambaye amerithiwa na Vilanova aliyekuwa msaidizi wake.

KOCHA mpya wa Barcelona, Tito Vilanova amekiri kwamba wanasaka mabeki kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao katika kipindi hiki cha usajili.
Vilanova amethibitisha kwamba watasajili mabeki mara dirisha la usajili litakapofunguliwa rasmi Julai 1.
"Ni kweli kwamba tunataka kusajili beki, tuna matatizo katika eneo hilo hadi tukalazimika kuwazoesha wachezaji kucheza nafasi hizo," alisema.
"Tunataka beki wa kushoto na beki wa kati. Mbele kwenye ushambuliaji msitarajie tutaleta mtu mwingine. Mwaka huu Villa, Alexis na Pedro walikuwa majeruhi, lakini msimu ujao tunatarajia watakuwa poa. Pia tunao yosso Cristian Tello na Isaac Cuenca."
Vilanova pia alikanusha uvumi unaomhusisha Dani Alves na mipango ya kuihama klabu hiyo, akimuelezea beki huyo wa kulia wa Brazil kama "mmoja wa watu muhimu zaidi kikosini" na akasema pia hawana mpango wa kumuuza kiungo Seydou Keita.

No comments:

Post a Comment