Saturday, June 16, 2012

Mourinho: Hispania chezeni kama Real, sio Barca

Jose Mourinho (kushoto) akizinguana na kipa wa Barcelona, Victor Valdes.

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amefadhaishwa na madai kwamba timu ya taifa ya Hispania inategemea mafanikio ya klabu ya Barcelona.
Mourinho amesisitiza kuwa ni Real ndio wanaotawala katika kikosi cha kocha Vicente del Bosque.
"Mnazungumzia Hispania na Barcelona lakini timu ya taifa ya Hispania ina wachezaji watano pia kutoka Real Madrid," Mourinho aliwaambia wanahabari.
"Sijui kwanini mnachanganya mambo hayo kwa sababu hayo ni mambo mawili tofauti.
"Barcelona walikuwa mabingwa wa Hispania. Narudia tena 'WALIKUWA' mabingwa wa Hispania, na hakuna cha zaidi."


No comments:

Post a Comment